Kwa nini mwanilaumu na roho kampenda yeye? Kwa nini mwanishtumu na macho kajichagulia? Si haki kabisa. Mimi mwenyewe nishaamua na moyoni ashaingia. Niacheni niringe naye. Ikiwa penzi ni wazimu jamani niacheni niugue. Hata mkinidhalilisha; sitotengana na aliyenipenda. Niacheni nitambe na niliyetunukiwa. Katu sitaachana naye, kwa sababu moyo kamteua.