Kwa nini mwanilaumu
na roho kampenda yeye?
Kwa nini mwanishtumu
na macho kajichagulia?
Si haki kabisa.
Mimi mwenyewe nishaamua
na moyoni ashaingia.
Niacheni niringe naye.
Ikiwa penzi ni wazimu
jamani niacheni niugue.
Hata mkinidhalilisha;
sitotengana na aliyenipenda.
Niacheni nitambe
na niliyetunukiwa.
Katu sitaachana naye,
kwa sababu moyo kamteua.